Mawasiliano

+255 653 407 894

Email

admin@njiapanda.com

Muda wa Kazi

Mon - Sat: 7AM - 7PM

Student’s management system for Advanced Level Tanzania Education Grading System

Ingia kwenye Mfumo kwa kuandika username ‘admin’ na password ‘admin’ then press Login

Interface ya kwanza baada tu ya Kulogin kwenye Advanced Student Management System

Hapa unaziona kazi zote zinazoweza kufanyika katika mfumo huu kwa pamoja.

Kazi zote zinafanyika katika menue zinazoonekana hapo juu kama ifuatatavyo:

1-USAJILI WA WANAFUNZI NA WATUMIAJI WA MFUMO AU KUIMPORT MAJINA YA WANAFUNZI KUTOKA KWENYE EXCEL.

Mfumo unatoa nafasi ya kusajili mwanafunzi mmoja mmoja, kuweka wanafunzi wengi ambao wapo kwenye excel pamoja na kuwabadilisha majina au kuwaona pale inapokuwa kuna ulazima wa kufanya hivyo, Futatilia video hapo chini kwa ufafanuzi zaidi.

2. KATIKA MFUMO PIA UTAONGEZA MADARASA, MASOMO PAMOJA NA KUHAMISHA WANAFUNZI KUTOKA DARASA MOJA HADI JINGINE

Uhamisho wa darasa moja hadi lingine mwisho wa mwaka na usafishaji wa data za masomo kwa undani zaidi tizama video inayohusiana na sehemu hii hapa chini.

3- UINGIZAJI RAHISI WA DATA ZA MITIHANI NA UUNGANISHAJI WA MITIHANI YA PRACTICAL NA THEORY AU PAPER1 NA PAPER2

Katika mfumo huu uwekaji wa data ni rahisi sana unaweka kwa kufuata Combination ya mwanafunzi pia unaweza kuunganisha masomo yenye paper1 na paper2 kwa wepesi kabisa, pia kubadilisha Alama za mitihani baada ya kuwekwa (kama wewe ni Administrator)

4.UMILIKI WA LOGO NA VICHWA VYA HABARI KATIKA PRINTOUT ZAKO UNAWEZEKANA PIA.

Baada ya kudownload mfumo huu utaona unazo logo na vichwa vya habari tofauti na shule yako hapa kuna maelekezo namna ya kubadilisha ili iweze kuprint repoti zenye logo yako na vichwa vya habari vilivyo na jina la shule yako halisi.

5. UTOAJI WA MIKEKA (EXAMINATION SCORESHEET) BAADA YA KUWEKA LOGO YAKO NA VICHWA VYA HABARI VINAVYOHUSU SHULE YAKO.

Baada ya kubadilisha logo sasa unaweza kuprint mikeka kwa namna yoyote unayotaka ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini kwa njia ya division, grades pamoja na Gpa kwa pamoja angalia video hapo chini kwa maelekezo zaidi.

6-TOA AU PRINT RIPOTI YA MWANAFUNZI ITAKAYOKUWA NA MAMBO YOTE MUHIMU ANAYOHITAJI KUJUA MZAZI.

Ripoti kwa ajili ya maendeleao ya wanafunzi kuhusu Taaluma, nidhamu na michango husika kama ipo pamoja na maoni ya mwalimu wa darasa, mtaaluma pamoja na mkuu wa shule kuhusiana na mwanafunzi yote hupatikana pamoja. Tizama video sinazofuata kwa ufafanuzi zaidi.

7-CHAPISHA RIPOTI KWA NJIA YA MOJA KWA MOJA

Baadhi ya nyakati ikiwa kila muhusika ameshaingiza data zake kwenye mfumo unaweza kuprint ripoti kwa kutumia Link ya automatic ambapo computer itafanya hivyo moja kwa moja.

NAMNA YA KUWEKA PROGRAM HII NA KUITUMIA KWENYE SHULE YAKO

 1. Download Server yetu hapa
 2. Angalia namna ya kuweka server kwenye computer yako
 3. Download Mafaili ya mfumo hapa
 4. Angalia namna ya kuweka mafaili na kuanzisha Mfumo.
 5. Namna ya kuanza kusajili wanafunzi au kuweka kutoka kwenye excel
 6. Angalia namna ya kusajili watumiaji katika Mfumo
 7. Class and Subjects management
 8. Students score entry [uingizaji wa Marks za mtihani au test]
 9. Customization – Tengeneza logo yako na uweke taarifa Printout zako.
 10. Scoresheet au Kuprint Mikeka aina zote
 11. Kuprint repoti za wanafunzi
 12. Kuweka data za ziada kwa ajili ya kuprint zinazotakiwa.

Kwa msaada au kuuliza lolote usisite kuwasiliana nasi: 0653 407 894. Ahsante