Mawasiliano

+255 653 407 894

Email

admin@njiapanda.com

Muda wa Kazi

Mon - Sat: 7AM - 7PM

Namna ya kudownload

 1. Ili utumie template hii anza kwa KUBOFYA HAPA ili uweze kuwa na template hii au sample hii kwenye computer yako.
 2. Kama unahitaji file la moja kwa moja ambalo unadownload moja kwa moja na kuweka kwenye desktop ya computer yako BOFYA HAPA-2

Baada ya Kudownload

 1. Kama umedownload kutoka katika maelekezo no-2 weka file lako kwenye desktop.
 2. Tengeneza Folder lako uweke ndani yake faili hilo na ulipe jina la darasa kwa Mfano FormI, FormII, FormIII na FormIV kwa hiyo utakua na mafaili manne ambayo yote yanafanana bali yanatofautiana majina tu
 3. Fungua sasa faili lako moja mfano Form One na litaonekana kama ifuatavyo:
Click sehemu iliyoandikwa Enable Content ili uweze kuendelea katika hatua inayofuata

3. Baada ya Kuclick Enable Content itafungua box nyingine ambayo itakuruhusu uingize password kama ifuatavyo:

Ingiza Password yetu kwa kuandika neno njiapanda kwa herufi ndogo na kisha bonyeza Click here to Login the System

4.Baada ya kufungua kwa hizo password Template yako itaonekana kama ifuatavyo:

Hapa utaanza kuweka majina (Kutype) Moja baada ya nyingine kama inavyoonekana hapa na kila darasa litakuwa na File lake ndio maana tumeweka mafaili manne ina maana kila darasa na file lake ukishaweka majina yote basi utasave na kuclose.

5. Njia nyingine ya kuweka majina ya wanafunzi katika Excel yetu hii ni kucopy majina kutoka kwenye file la zamani na kuweka katika file letu hili kama ifuatavyo:

Namna ya kukopi kutoka kwenye file la zamani. Select majina yote kisha Press Copy.

6.Paste kwenye template yetu kama inavyoonekana hapa chini na hakikisha vertical bar (ya upande wa kulia ipo juu) ili uselect row ya kwanza kabisa kama inavyoonekana hapa chini.

7.Baada ya kuhakikisha umechagua row ya kwanza kabisa kama inavyoonekana hapo juu basi Paste zile data ulizocopi hatua ya tano 5 hapo juu kama ifuatavyo

Utaclick Paste au Tumia CTrl+V (Unaclick Ctrl bila kuachia unapress V)

8. Baada ya kupaste Au Kuandika majina yote Utaanza kuingiza Marks za kila somo (Somo la kwanza kabisa litakalokuwepo ni Civics)

9. Baada ya kuingiza Alama zote katika somo la mwanzo utachagua somo lingine kwa kufuata hatua zifuatazo:

Sehemu iliyoandikwa Select Subject to Fill Score hapo utachagua somo lolote na kuweka alama zale zote kama inavyoonekana hiyo menyu hapo juu

10. Evaluation (Tathmini ya Alama za somo ulizoweka) Baada ya kuweka alama zote za somo utaclick sehemu iliyoandikwa Evaluation pembeni ya jina la somo utaona Tathmini ya hilo somo imefanyika kama imavyoonekana hapo chini

11.Subject Evaluation. Tathmini hiyo inafanyika katika category nne. Kwanza katika nusu muhula (Mid term1), Terminal, Nusu muhula wa pili (Mid term2), na Annual. Pia endapo utataka kufanya tathmini kwa mwaka mzima wa somo husika inawezekana. Angalia maelekezo ya tathmini hapo chini ya picha inayofuata.

Kwanza – Click Clear All Evaluation present ili ufute evaluation yoyote usiyoitaka
1. Tathmini ya robo ya 1 Click Mid term1 –> January – March
2. Tathmini ya robo ya 2 Click Terminal —-> April -Terminal exams
3. Tathmini ya robo ya 3 Click Midterm 2 —-> July – September
4. Tathmini ya robo ya 4 Click Annual —–> October – Annual Exams
5. Tathmini ya mwaka Mzima Click General Compilation——> January – Annual exams
6. Baada ya kufanya Tathmini tafadhali Click Clear all Evaluation present, Pia fanya tathmini ya kila somo kabla ya kuprint report Maana baadhi ya data zinahitajika kwenye report.

12.Baada ya kufanya Tathmini ya kila somo na kufuta tathmini hizo baada ya kuprint sasa Unaweze kufungua Scoresheet au Mkeka kwa lugha tuliyoizoea. utaclick sehemu iliyoandikwa Printing & Editing kama inavyoonekana hapa chini kisha utachagua Open Scoresheet

13. Scoresheet au mkeka utafunguka kama unavyoonekana katika picha hapa.

Muonekano wa Mkeka kabla ya kujazwa data ndani yake.

14. Ili kujaza mkeka data unazotaka kuona, maana pengine una data kwenye template yako za january, february nk, Hivyo utachagua data unazotaka kuona kwenye mkeka kwa kuclick sehemu iliyoandikwa Click to view real data kama ifuatavyo:

Picha inayoonesha menue ya kupata kuangalia data mbalimbali zilizopo kwenye system.

15. Baada ya kuchagua Get real January Score au mwezi wowote ambao data zake zimo kwenye template utaona mkeka umejaa data kama unavyoonekana hapa chini:

Mwonekano wa Mkeka au Scoreheet.

16. Mkeka au scoresheet itaonesha position za wanafunzi kwa mtiririko wa majina kama ulivyoyaweka au kusajili, Lakini ikiwa unataka kupanga kuanzia wa kwanza kwa ufaulu au kufeli utaclick sehemu iliyoandikwa Conditional View kama ifuatavyo:

17. Hapo utachagua According to better performance au Poor performance na kisha wanafunzi watajipanga upya kwenye mkeka kwa kufuata unachotaka kuona kwa muda huo kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini.

Wanafunzi wamepangwa kwa kufuata ubora wa kufaulu kwa wastani wao.

18. Baada ya kuziona data zako sasa unaweza kuprint ili wanafunzi wazione marks zao kwenye mbao za matangazo kwa kuclick sehemu iliyoandikwa Printing & Back home.

Hapa utaprint kwenye printa iliyounganishwa na computa yako moja kwa moja. Baada ya kuprint Click tena hapo palipoandikwa Printing & Back Home uclick tena sehemu iliyoandikwa Back to academic Home kwa ajili ya Kuprint report Kama zinatakiwa

19. Hatua ya mwisho ni utayarishaji wa ripoti za matokea ya wanafunzi darasani. Ambapo mambo yafuatayo yana takiwa kuzingatiwa.

 • Masomo yote yawe yamefanyiwa Evaluation/Tathmini kufuatana na ripoti zinazotakiwa muda huo. Kwa mfano Midterm1 report ndizo zinatakiwa hivyo masomo yote yawe yamefanyiwa evaluation kwa kuzingatia chaguo la midterm1.
 • Taarifa za muhimu zinazotakiwa kwenye ripoti zijazwe katika system kwa kufungua ukurasa maalum kwa kuclick sehemu iliyoandikwa Prepatarion of Exams Scoresheet na kuhakikisha umejaza kila jambo la muhimu lililopo hapa na kusave baada ya kujaza

20. Page itakayofunguka ili ujaze taarifa zote za muhimu zinazotakiwa kwenye ripoti ni hii hapa chini

Ili repoti iwe nzuri na ya kupendeza katika muonekano hakikisha unapopewa nafasi ya kuandika maneno unaandika maneno yanayotosha katika nafasi bila ya kuzidi au kupungua sana, Mfano nafasi ya mistari miwili unaweza kuandika kwa mstari mmoja na nusu na wala sio mitatu au mmoja. (Poleni hua napenda vitu smart) Baada ya kuadika Save tafadhali

21. Baada ya kuandika Comments zote, tarehe za kufunga na kufungua na mengineyo. Sasa click Back to home Page huko home sasa click sehemu iliyoandikwa Printing & Editing Kisha kwenye hiyo menu Click sehemu ya mwisho kabisa iliyoandikwa Preparation of Student’s Report itafunguka kama hivi hapa chini.

22. Hapa sasa utaclick sehemu iliyoandikwa Click to Get real Data ili uchague ni aina gani ya ripoti unayotaka kuprint, na menue yake ni kama hii.

Hapa utacahgua kulingana na mahitaji ya wakati huo, Kumbuka mpaka unafika hapa uwe umwshafanya Subject Evaluation mojamoja na umeclear Present data Baada tu ya cuclick chagua lako utaona data zimejaa kwenye mkeka huo.

23. Baada ya data kujaa kwenye Mkeka huo utaclick sehemu iliyoandikwa Start Printing Page to page na utaona Page yako inafunguka kama hivi hapa chini.

24. Namna ya kuprint. Ili uprint report zako kwa ufanisi utaclick Print Now Baada ya kuwa umeunganishwa kwenye printa (Default Printer)

 • Print Now itafungua kibox kinachokutaka ujaze unahitaji kuprint kuanzia rekodi ya ngapi mpaka ya ngapi .
 • Kwa Mfano nahitaji ripoti moja tu ya saba baada ya kuliona jina ni la saba kwenye mkeka wa kumprint repot (Mkeke no 22 kwenye SN-serial number) Basi utajaza kwenye kibox 7 kisha uytabonyeza OK kibox chapili utajaza hiyo hiyo 7 (Tafsiri yake 7 mpaka 7)
 • Ikiwa unataka kuprint mwanafunzi wa kwanza mpaka kumi utabonyeza Print Now kisha Kobox cha kwanza utajaza 1 kisha OK then kibox cha pili utajaza 10 Template yetu itaprint report zote.
 • Mwonekano wa report ni kama ifuatavyo

A

Kwa maswali yoyote usisite tuwasiliane +255 653 407 894 Au njiapanda25@gmail.com