Mawasiliano

+255 653 407 894

Email

admin@njiapanda.com

Muda wa Kazi

Mon - Sat: 7AM - 7PM

Huu ni mfumo mpya ulioboreshwa tangu mwaka 2014 na umekua ukifanyiwa marekebisho ya mara kwa mara ili kukidhi mahitaji ya wafanya biashara wa kada mbalimbali. Hivi sasa mfumo huu unapatikana katika website yetu hii na kama mtu anahitaji kuona unavyofanya kazi tutamuunganisha kwa kumsajili ili aweze kufanya majaribio kadhaa kabla ya kuomba kuwekewa mfumo huu katika eneo la biashara yake.

Biashara Smart Suluhisho la taarifa za Biashara yako kuanzia kubwa na ndogo pia.

MAZINGIRA YA KUTUMIA BIASHARA SMART

Mfumo huu unaweza kufanya kazi katika hali zifuatazo:

  • Njia ya mtandao: – ikiwa simu yako ina uwezo wa kuingia kwenye mtandao kwa kasi ya kawaida unaweza kufanya mauzo kwa mtandao kwa kutumia simu yako na kuona makusanyo yako na stoo ukiwa sahemu yoyote.
  • Kwa njia ya mtandao wa kazini kwako tu: – Njia hii haihitaji kununua bando la internet bali utatumia kifaa maalum (router) ambapo watu wa eneo lako la kazi ndio pekee watatumia mfumo bila ya kutoa nje taarifa na utatumia simu yako au computer.
  • Kwa njia isiyokuwa ya mtandao kabisa: – Mfumo utawekwa kwenye computer moja kisha kila kitu utapaswa kufanyia hapo kuanzia utoaji wa risiti mpaka uangaliaji wa mapato na matumizi

MANUFAA AU FAIDA YA BIASHARA SMART

Utaweza kuona Stoo ya Biashara yako yote na hali ya stoo kwa ujumla kama vile:

a) Kujua ni Bidhaa gani zinauzwa zaidi katika biashara yako katika kipindi chochote utakachochagua katika mfumo

b) Ni Bidhaa zipi zimebaki chache katika biashara yako na zinahitajika

c) Ni bidhaa zipi zinakaribia kufikia Expire yake ili uziondoe kwa kuzifanyia discount au kwa njia yoyote ya kibiashara

Utaweza kuangalia mapato yako kwa namna zifuatazo

a) Mapato ya kila siku

b) Mapato kwa kipindi maalum kama wiki, mwezi mwaka nk

c) Faida katika kila siku au wiki [kama wewe ni meneja wa Mfumo sio mtumiaji wa kawaida ] kwani mtumiaji wa kawaida anaona mapato tu bila ya faida

Utaweza kuona matumizi yako yote yaliyopo katika biashara yako kwa namna ifuatayo:

a) Matumizi ya kila siku ya kawaida

b) Matumizi ya manunuzi ya bidhaa zinazokwisha

c) Jumla ya matumizi kwa kipindi chochote unachotaka kama wiki, mwezi au hata mwaka

>Utaweza pia kuangalia madeni ya wateja wako kwa namna ifuatavyo:

a) Madeni yote kwa ujumla kwa kipindi chochote utakachotaka

b) Deni la kila mteja mmojammoja

c) Jumla ya madeni yote kwa kipindi chochote unachotaka

d) Ulipaji wa madeni kwa ujumla na taarifa zake zote

e) Kuangalia Bidhaa zote mteja alizowahi kununua kwako kama atahitaji

SASA TUONE NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WETU MOJA KWA MOJA.

  1. Kuingia kwenye Mfumo kama Meneja au Mtumiaji mkuu
  2. Usajili wa Bidhaa kwenye Mfumo na kuziangalia
  3. Uuzaji wa Bidhaa zilizosajiliwa
  4. Wateja na wasambazaji wa bidhaa
  5. Mapato na Matumizi kwa kutumia Mfumo huu
  6. Kwa majaribio Tuma sms whatapp 0653 407 894 upewe jina la kutumia na password kisha Click Hapa kuingia. Ahsante

MASWALI NA MAJIBU NAMNA YA KUTUMIA BIASHARA SMART